Featured post

Historia ya VW Beetles (people's car)

Hizi ni gari zinazovutia sana macho ya watu wengi,kwa Tanzania zimepotea kwa kiasi kikubwa kutokana na kufurika kwa magari ya kisasa kutoka...

Friday 5 October 2018

Car maestro. Jinsi ya ku-drift

Kwa kiswahili ni maarufu kama "kupiga norinda" baadhi ya madereva wanaujuzi wa kuchezea gari na kulifanya lizunguke mduara yaani nyuzi 360° au nusu duara nyuzi 180°, pia wapo wanaoweza kufika 90° tu.

                   
Kuna aina nyingi za kupiga norinda ila inafaa uchague njia sahihi na kwa mazingira sahihi pia na chombo sahihi ukizingatia Usalama kwanza.

Drifting pia unaweza kufanya wakat unakunja kona ya U-turn/Au round about.. Ufundi huo unajulikana kitaalam kama Counter steering..(unakunja kushoto gari inaenda kulia) yote hutokea baada ya tair kupoteza uwezo wa kushika ardhi kwa ufasaha.. (Loss of traction)

Haya.... Siku zote tunaambiwa "practice makes perfect" inafaa kuwa na mazoezi ya mara kwa mara.. Ili uongeze hali ya kujiamini na umahiri zaidi..

Hesabu zimetawala hapa.. Na sio kukariri bali ni uzoefu na kucheza motion ya gari kwa ufasaha.

Njia za kufanya drifting

Hii ni njia ya kutumia Handbrake.. Unaondoka na spidi ya kiasi alafu unavuta hand brake kwa muda wa sekunde kadhaa tu wakat huohuo ukipindisha usukani wako...kama ukipindisha upande wa kushoto gari itaenda kulia na kama ukipindisha kulia gari itaenda kushoto.. Ukisaidia na kukanyaga mafuta kwa mbaali....

Njia ya pili.. Hii unakanyaga klatch huku unakanyag na mafuta mpaka Rpms zipande kwa kasi alaf unaachia klachi kwa  haraka.. Hapo utasababisha tairi za nyuma kupoteza uwezo wa kushika ardhi pia kuzunguka kwa haraka sana.. Hivyo unawez kuongezea kwa kukanyaga mafuta kwa makadirio

Pia njia ya mwisho kabisa.. Ni kukanyaga mafuta kwa nguvu katika kona... Yaan ukiikaribia kona kanyaga mafuta kwa nguvu.. Tairi za nyuma zitapoteza uwezo  wa kushikamana na ardhi hivyo gari itakuwa katik drifting mode (Hii njia inashauriwa uwe na gari yenye horsepower kubwa kuanzia 240)


Historia kwa ufupi.. Drifting imeanzia nchini JAPANI katika miaka ya 1970.. Na kuuteka ulimwengu wa leo.. Next article Nitazungumzia kuhusu "Pararell parking"
#Usalama  kwanza

#Kuwa na gari imara

#Chukua tahadhari..