Featured post

Historia ya VW Beetles (people's car)

Hizi ni gari zinazovutia sana macho ya watu wengi,kwa Tanzania zimepotea kwa kiasi kikubwa kutokana na kufurika kwa magari ya kisasa kutoka...

Thursday 12 July 2018

Historia ya VW Beetles (people's car)


Hizi ni gari zinazovutia sana macho ya watu wengi,kwa Tanzania zimepotea kwa kiasi kikubwa kutokana na kufurika kwa magari ya kisasa kutoka katika nchi mbalimbali ikiwemo JAPAN kuwa ndio kinara wa kuleta gari nyingi sana..

Chimbuko la VW

huwezi kuamini,ila ukweli ndio huu,katika miaka ya 1924 Mwamba wa DUNIA Adolf Hitler alipata wazo la kutengenezwa kwa gari hizi akiwa GEREZANI..
Hitler aliwaza mengi ikiwemo kupunguza Tatizo la ajira katika nchi yake,pia Gari hizi zingeweza kununuliwa na watu wengi hasa wale wenye Uchumi wa kati na wachini pia,ndio maana VolksWagen huitwa (peoplea's car) yaani 'Gari ya watu'.
ilipofikia miaka ya 1933 Chama cha NAZI kiliingia madarakani na Hitler jambo lake la kwanza ni kuwepo kwa barabara maalum kwa ajili ya magari,na alifanikiwa kufanya hayo na ndoto yake ilikamilika MWAKA 1939.

Zoezi zima la KUUNDWA kwa VW

Ferdinand Porsche,ambaye ndiye mmiliki wa kampuni ya Kubuni na kudizaini magari,iliyopo STUTTGART Germany alipewa kibarua kizito na Adolf hitler akamilishe ndoto yake ya kutengeneza gari muhimu ndani ya miezi kumi.. kibarua hicho alipewa 1934... na hakumuangusha Bosi wake alidizain vile Hitler alivyotaka...

yafuatayo ni maagizo aliyompa bwana ferdinand Porsche...

-gari inatakiwa iwe na uwezo wa kukimbia; 62Mph.
-gari iwe na uwezo wa kwenda miles (maili) 45 kwa lita 5.
-gari inatakiwa iwe na injini yenye mfumo wa kupoza kwa kutumia Hewa.
-pia iwe na uwezo wa kusafirisha watu wazima wawili na watoto watatu.
-na jambo la mwisho alilosisitiza ni kuwa gari lazima iuzwe bei isiyozidi £8.

UCHAMBUZI WA VW beetle (Overview)
>Adolf hitler alisisitiza matumizi ya injini inayopoozwa kwa upepo kuliko injini inayopoozwa kwa Maji kwasababu injini inayopoozwa kwa upepo ni Nyepesi kulinganisha na hii injini nyingine..
>Volkswagen Beetle (1938-1979) Kipindi hicho chote, ilishika nafasi ya pili kwa kuwa ndiyo Gari iliyouzwa kwa wingi Duniani kwa ujumla
>jumla ya Magari milion 21 yalitengenezwa Duniani kwa ujumla
>Hizi gari zina tambulika kuwa injini yake inakaa nyuma,hivyo kumpa dereva uwezo wa kukata kona kiurahisi bila ya kutumia nguvu nyingi,pia mbele kuna nafasi inayotumika kuweka mizigo pia katika siti kwa nyuma kuna nafasi kubwa tu ya kuweka mizigo mbalimbali.
>1959 katika bara la AMERIKA ilishika nafasi ya kwanza kwa magari ya kigeni yaliyouzwa barani humo..
MATOLEO mbalimbali ya BEETLES
(inapaswa kuzingatiwa kuwa kabla ya vita ya pili ya Dunia Kila nchi Barani ulaya ilijipanga kikamilifu.. hali iliyochangia Hitler kuimalisha safu yake ya jeshi kwa kuundwa kwa beetle maalum kwa matumizi ya jeshi tuu... na ni kwa wanajeshi walio na beji ya VIP.. gari hii ni Kommandeurwagen or type 87  Toleo lijalo nitaichambua gari hii kiundani zaidi maana ina maajabu ya kipekee)
1-Type 82 Kubelwagen ---boat mode
2-Type 166 Schwimmwagen
3-Kommandeurwagen or type 87  
zipo zingine nyingi
-Volkswagen AutoStick 1967 ulaya/1968 Marekani (kama tunavyowajua wamarekani wanavyopenda URAHISI, miaka yote nyuma beetles zilikuwa ni (manual) ila kipindi hiki waliona watoe beetle yenye uwezo wa kutumika kama manual na automatic gari hizi zilikuwa hazina (clutch pedal)..
-Super Beetle ilitengenezwa 1971 mpaka 1979
-Beetle Convertible hii iliundwa katika miaka ya 1953

ingawa gari hizi zinatambulika kuwa na nguvu ndogo,zilipendwa na wengi kwa sababu ni rahisi kuzimudu katika masuala ya mafuta,vipuri (spea) ni rahisi kununuliwa na mambo mengine mengi.


Kupotea Kwa Beetles katika Ramani ya DUNIA
-HADI kufikia miaka ya 1970's ushindani wa kutengeneza magari ya kiuchumi (yasiyotumia mafuta mengi) ulizidi kwa kasi kutokana na wamerekani na wajapani kuingilia soko hili la magari kwa nguvu kubwa sana

wamerekani walikuja na aina mpya ya gari ambayo ni Chevrolet Vega na Ford Pinto ambazo zilipendwa na atu wengi kutokana na kutumia mafuta kwa kiasi kidogo,mauzo ya beetles yalishuka kwa asilimia 50%

viwanda mbalimbali viliacha na vingine kupunguza uzalishaji wa beetles nchini ujerumani hadi kufikia miaka ya 1979 ingawa walichechemea kutengeneza gari hizi hadi 1980 ili kukamilisha oda mbalimbali walizopokea duniani kote.

Mwisho..
>>>> Wafanyabiashara na wateja wengi wa beetles waliibukia nchini MEXICO na kuendelea kutengeneza gari hizi miaka ya 1981 kufikia idadi ya gari milioni 20 kutengenezwa katika Ardhi ya mexico..
hadi kufikia hivi leo MEXICO ndio nchi Pekee inayotengeneza gari aina Beetles
na gari hii iliteka hisia za wengi na kupelekea kupigiwa kura na wananchi wa MEXICO kuwa ndio gari pendwa ya nchi yao kuliko gari nyingine yoyote ile katika karne Hii.




No comments:

Post a Comment