Featured post

Historia ya VW Beetles (people's car)

Hizi ni gari zinazovutia sana macho ya watu wengi,kwa Tanzania zimepotea kwa kiasi kikubwa kutokana na kufurika kwa magari ya kisasa kutoka...

Friday 13 July 2018

VIFAA MAALUMU VINAVYOWEZA KUGUNDUA (Tochi) (speedGuns/Speed Radar)

Maendeleo ya sayansi na teknolojia yamekuwa kwa kasi na kuibuka ushindani wa mambo mengi yanayotawala maisha ya binadamu kwa kiasi kikubwa,
mashindano hayo yamepelekea vyombo vya usalama katika nchi mbalimbali kutumia pesa nyingi ili wawe na teknolojia mpya itakayowalahisishia kazi ya kukamata wahalifu mbalimbali,pia wahalifu nao hawako nyuma wao ndio vinara wa kugundua teknolojia mpya ili wasiingie katika mikono ya polisi..

RADAR DETECTORS/vigunduzi vya TOCHI
Kuanzia miaka ya 1970 vifaa hivi vinavyotoa taarifa ya kuwepo ASKARI mwenye Tochi au Tochi iliyotegeshwa kwa dereva aliye kwenye mwendokasi  hivyo dereva huyo kupunguza mwendo wa chombo chake..

kila miaka inavyozidi kwenda Vifaa hivi (TOCHI) vinafanyiwa marekebisho zaidi ili kukamata madereva wasio fata sheria za barabara (mwendokasi)

kwa sasa kuna toleo jipya la hivi vigunduzi vya tochi ambavyo vinaharibu taarifa iliyotakiwa kuchukuliwa na tochi,hivyo tochi kusoma spidi 0 ingawa gari imepita ikiwa na mwendo mkali hata kufikia 180/kph

kwa nchi zilizoendelea zimetoka katika kutumia TOCHI zinazopima kwa kutumia nyenzo ya RADIO WAVES..na kuhamia katika Infraled LIGHT (TOCHI aina ya LIDAR GUN) ambayo hupimwa na LIDAR DETECTOR pekee..
SPEED GUN /speed radar (TOCHI)
Askari wa barabarani anayetumia Tochi(LIDAR GUN) huweza kusoma mwendokasi wa gari husika hata ikiwa umbali wa (mita910) sasa hivi vigunduzi vya LIDAR detector vina uwezo wa kuchanganya (Tochi LDAR GUN) na hatimaye kufeli kusoma spidi husika.. hata kama gari imepita na 180kph kwa polisi itasoma 0kph.


JE SHERIA INARUHUSU VIFAA HIVI?

Jibu ni HAPANA.. na NDIO kwa wakati mmoja, kuna nchi mbalimbali zinaruhusu kumiliki kifaa hiki ila Hauruhusiwi kukitumia katika gari,zipo nchi nyingine hauruhusiwi kumiliki wala kutumia katika gari.

nchi za ukanda wa scandnavia zimeweka sheria kali kutokana na MATUMIZI ya vifaa hivi ikiwemo FAINI kubwa kwa dereva atayegundulika pia kutaifishwa kwa kifaa endapo kitakamatwa na askari wa usalama barabarani...
moja ya kifaa madhubuti kinachotoa taarifa kwa dereva iwapo mbele kuna ASKARI mwenye tochi au TOCHI iliyotegeshwa(radar detector) 


 VIFAA BORA VYA UGUNDUZI WA TOCHI (SpeedRADAR Detectors)
#1 : Uniden R1 & Uniden R3 Radar Detectors
BEI: $299 kwa  R1,
      ; $399 kwa R3 Radar Detector

#2 : Valentine One Radar Detector /w V1Connection or V1Connection LE
BEI: $399 kwa V1,
      ; $49 kwa Bluetooth module,katika iphone/android bure

#3 : Escort Redline EX Radar Detectors
BEI: $599

#4 : Escort Max 360 Radar Detector
BEI: $649, katika iPhone/Android bure ila kwa matumizi kwa ufanisi zaid
 BEI;$49/Ada ya mwaka.

#5 : Radenso XP & Radenso SP Radar Detectors
BEI: $249 kwa SP, 
      ;$399 kwa XP Radar Detector

#6 : Escort iX Radar Detector
BEI: $399

#7 : Radenso Pro M Radar Detector
BEI: $549

#8 : Uniden DFR7 & Uniden DFR6 Radar Detectors
BEI: $399 kwa DFR7,
      ; $299 kwa DFR6

#9 : Escort X80 Radar Detector
BEI: $299

#10 : Whistler CR93 & Whistler CR88 Radar Detectors
BEI: $279 kwa CR93, 
      ;$229 kwa CR88

Honorable Mention: Cobra DSP-9200BT Radar Detector
BEI: $299





No comments:

Post a Comment