Featured post

Historia ya VW Beetles (people's car)

Hizi ni gari zinazovutia sana macho ya watu wengi,kwa Tanzania zimepotea kwa kiasi kikubwa kutokana na kufurika kwa magari ya kisasa kutoka...

Monday 17 September 2018

JIFUNZE jinsi ya kupiga DEDE (wheeling)

(Salum Tony MONTANA) TZ
DEDE ni nini? je ni kitu kigeni kwa upande wako?
DEDE ni uwezo wa pikipiki (baiskeli pia) kuweza kusimama kwa kutumia tairi moja (la nyuma pekee) huku tairi la mbele likielea angani... na chombo hicho kuweza kutembeaa kwa kutegemea tairi hlo moja..

kila biker ana mbinu yake anayoipenda  katika kufanikisha hili.. je ni mbinu zipi.. ?? endelea....

kuna wanao tegemea nguvu ya Engine.. (injini) kupaisha pikipiki juu (POWER WHEELIE)
kuna wanaotumia Clutch na msaada wa nguvu ya injini (engine revs)  kwa kiwango cha juu kuipaisha pikipiki juu (CLUTCH WHEELIE)


power wheeling...
hii mbinu hutumiwa na baadhi ya watu,ila ni rahisi kuanguka ikiwa (bado hujaiva)
apa unakaa katika ncha ya siti yako (karibia na mwisho wa siti)  ili uzito ukae nyuma na ugandamize pikipiki.. baada ya kufanya hivyo mikono yako unatakiwa usukume usukani wa pikipiki yako kama unaingiza chini.. (unabinya usukani mpaka suspension ziingie ndani kiasi) wakati huo huo pikipiki inaenda... anza na (gear #1) binya usukani...alafu achiaa huku unavuta mafuta kwa kasi...
hivyo kuifanya tairi iache ardhi na kunyanyuka juu.. kwakuwa umekaa mwishoni mwa siti unaipa pikipiki uzito kwa nyuma, hivyo mbele ni kwepesi ukizingatia tairi limepanda juu basi.. balance mafuta... ukiona huwezi kuhimili kwa muda mrefu badili gear na uingie gear #2.. #3.. pia inashauriwa kutocheza mbali na breki yako ya nyuma..,
 hii itakufanya ujihakikishie ujasiri na usalama.. ukiona imekuzidi ,kanyaga hiyo breki basi tairi linashuka kiasi au chini kabisa.. BREKI MUHIMU
(hii mbinu inahusisha KASI... bila kasi tairi halinyanyuki kirahisi)

Cluth wheeling...........
anza na gear #1.. vuta mafuta.. kiasi kandamiza  usukani wako.. minya klachi (huku unavuta mafuta)na uiachie  hapo hapo.. bila kupunguza mafuta... tairi litapanda juu... kutokana na kuishtua pikipiki ambayo inajivuta kwa nguvu na kujiachia hivyo ule uzito uliopo nyuma unakusanywa na kuhamishwa kwa mbele hivyo tairi kuweza kuacha ardhi na kuelea angani.

sasa tafuta balance point...  huku unavuta mafuta kwa kuyapimia.. bila kusahau breki..(ya nyuma) pale unapoona inazidi kuja juu...
(kasi haizingatiwi sana.. ni best kwa wazee wanaopenda SLOW JAMS..."slow wheeling"
standing wheelie (Don ghb)TZ

unaweza kutumia manjonjo mbalimbali... 
kama KUSIMAMIA... (standing wheelie)
-kupiga mikasi (RINGI)..
Ringi (Salum Tony MONTANA) TZ
pia hata kushusha mguu mmoja chini..na nyingine nyingi.. yote yanawezekana..

JE naweza kutumia pikipiki yoyote kufanya mchezo huu???

JIBU ni ndio/hapana kwa wakati mmoja...
inafaa pikipiki yenye nguvu.. yenye uwezo.. yenye vifaa vilivyo bora na utimamu wa injini...
(slogan ya watu wa dede wanasema HAIKATAI).. wakimaanisha hakuna pikipiki inayowashinda kunyanyua...

Acrobatics (ahmed kalunde)TZ
ANGALIZO..
-hakikisha umevaa nguo nzito kujihami na michubuko ya hapa na pale
-hakikisha unafanya mchezo huu mbali na makazi ya watu.. au mbali na mkusanyiko wa watu (kama unajifunza)
-hakikisha umejikinga kichwa chako kwa kuvaa kofia ngumu..

ni HATARI lakini SALAMA..

sitting wheelie  (Chudy) TZ 
#DAR WHEELIE BOYZ respect
#Kaskazini wheelie boys respect..





unaweza kuuliza swali lolote tutakusaidia

10 comments:

  1. Hii n kweree joh Sisi ndo tunaanza kujifunzaa wakuu

    ReplyDelete
  2. Suspension ndo kitu gan

    ReplyDelete
  3. Sana naikubali

    ReplyDelete
  4. Kifo nakiona kabisa hapo kwenye maelezo 😂😂😂😂

    ReplyDelete
  5. mimi inawai kushuka kwanini

    ReplyDelete
  6. Respect and that i have a neat provide: Who Repairs House Windows Near Me average remodel cost

    ReplyDelete