Featured post

Historia ya VW Beetles (people's car)

Hizi ni gari zinazovutia sana macho ya watu wengi,kwa Tanzania zimepotea kwa kiasi kikubwa kutokana na kufurika kwa magari ya kisasa kutoka...

Monday 5 November 2018

Tujue NOS (Nitrous) na utendaji kazi wake.

Nitrous oxide inachangia kuongeza kiasi cha Oxygen katika mtiririko mzima wa uchomaji mafuta katika gari na kubadilisha mafuta gavi kuwa nguvu inayotumiwa na injini..

Pia hupooza chemba za kuchomea mafu

ta (combustion chambers) hivyo inatoa uwanda mpana kwa injini kujirahisishia uchomaji wa mafuta kwa kiwango stahiki na nguvu kuongezeka mara dufu

Hivyo basi Nos inasaidia kujaza hewa ya oxygen katika chemba za kulipua mafuta.., Jinsi hewa ya oxygen inavyojaa basi na kiwango cha mafuta kuchomwa katika chemba kinaongezeka maradufu vilevile.. Nguvu inaongezeka maradufu..

#njia nyingine inayoweza kuongeza ufanisi wa injini ni kuweka TURBOchargers au SUPERchargers..






Mtungi wenye NOS

Friday 5 October 2018

Car maestro. Jinsi ya ku-drift

Kwa kiswahili ni maarufu kama "kupiga norinda" baadhi ya madereva wanaujuzi wa kuchezea gari na kulifanya lizunguke mduara yaani nyuzi 360° au nusu duara nyuzi 180°, pia wapo wanaoweza kufika 90° tu.

                   
Kuna aina nyingi za kupiga norinda ila inafaa uchague njia sahihi na kwa mazingira sahihi pia na chombo sahihi ukizingatia Usalama kwanza.

Drifting pia unaweza kufanya wakat unakunja kona ya U-turn/Au round about.. Ufundi huo unajulikana kitaalam kama Counter steering..(unakunja kushoto gari inaenda kulia) yote hutokea baada ya tair kupoteza uwezo wa kushika ardhi kwa ufasaha.. (Loss of traction)

Haya.... Siku zote tunaambiwa "practice makes perfect" inafaa kuwa na mazoezi ya mara kwa mara.. Ili uongeze hali ya kujiamini na umahiri zaidi..

Hesabu zimetawala hapa.. Na sio kukariri bali ni uzoefu na kucheza motion ya gari kwa ufasaha.

Njia za kufanya drifting

Hii ni njia ya kutumia Handbrake.. Unaondoka na spidi ya kiasi alafu unavuta hand brake kwa muda wa sekunde kadhaa tu wakat huohuo ukipindisha usukani wako...kama ukipindisha upande wa kushoto gari itaenda kulia na kama ukipindisha kulia gari itaenda kushoto.. Ukisaidia na kukanyaga mafuta kwa mbaali....

Njia ya pili.. Hii unakanyaga klatch huku unakanyag na mafuta mpaka Rpms zipande kwa kasi alaf unaachia klachi kwa  haraka.. Hapo utasababisha tairi za nyuma kupoteza uwezo wa kushika ardhi pia kuzunguka kwa haraka sana.. Hivyo unawez kuongezea kwa kukanyaga mafuta kwa makadirio

Pia njia ya mwisho kabisa.. Ni kukanyaga mafuta kwa nguvu katika kona... Yaan ukiikaribia kona kanyaga mafuta kwa nguvu.. Tairi za nyuma zitapoteza uwezo  wa kushikamana na ardhi hivyo gari itakuwa katik drifting mode (Hii njia inashauriwa uwe na gari yenye horsepower kubwa kuanzia 240)


Historia kwa ufupi.. Drifting imeanzia nchini JAPANI katika miaka ya 1970.. Na kuuteka ulimwengu wa leo.. Next article Nitazungumzia kuhusu "Pararell parking"
#Usalama  kwanza

#Kuwa na gari imara

#Chukua tahadhari..


Monday 17 September 2018

JIFUNZE jinsi ya kupiga DEDE (wheeling)

(Salum Tony MONTANA) TZ
DEDE ni nini? je ni kitu kigeni kwa upande wako?
DEDE ni uwezo wa pikipiki (baiskeli pia) kuweza kusimama kwa kutumia tairi moja (la nyuma pekee) huku tairi la mbele likielea angani... na chombo hicho kuweza kutembeaa kwa kutegemea tairi hlo moja..

kila biker ana mbinu yake anayoipenda  katika kufanikisha hili.. je ni mbinu zipi.. ?? endelea....

kuna wanao tegemea nguvu ya Engine.. (injini) kupaisha pikipiki juu (POWER WHEELIE)
kuna wanaotumia Clutch na msaada wa nguvu ya injini (engine revs)  kwa kiwango cha juu kuipaisha pikipiki juu (CLUTCH WHEELIE)


power wheeling...
hii mbinu hutumiwa na baadhi ya watu,ila ni rahisi kuanguka ikiwa (bado hujaiva)
apa unakaa katika ncha ya siti yako (karibia na mwisho wa siti)  ili uzito ukae nyuma na ugandamize pikipiki.. baada ya kufanya hivyo mikono yako unatakiwa usukume usukani wa pikipiki yako kama unaingiza chini.. (unabinya usukani mpaka suspension ziingie ndani kiasi) wakati huo huo pikipiki inaenda... anza na (gear #1) binya usukani...alafu achiaa huku unavuta mafuta kwa kasi...
hivyo kuifanya tairi iache ardhi na kunyanyuka juu.. kwakuwa umekaa mwishoni mwa siti unaipa pikipiki uzito kwa nyuma, hivyo mbele ni kwepesi ukizingatia tairi limepanda juu basi.. balance mafuta... ukiona huwezi kuhimili kwa muda mrefu badili gear na uingie gear #2.. #3.. pia inashauriwa kutocheza mbali na breki yako ya nyuma..,
 hii itakufanya ujihakikishie ujasiri na usalama.. ukiona imekuzidi ,kanyaga hiyo breki basi tairi linashuka kiasi au chini kabisa.. BREKI MUHIMU
(hii mbinu inahusisha KASI... bila kasi tairi halinyanyuki kirahisi)

Cluth wheeling...........
anza na gear #1.. vuta mafuta.. kiasi kandamiza  usukani wako.. minya klachi (huku unavuta mafuta)na uiachie  hapo hapo.. bila kupunguza mafuta... tairi litapanda juu... kutokana na kuishtua pikipiki ambayo inajivuta kwa nguvu na kujiachia hivyo ule uzito uliopo nyuma unakusanywa na kuhamishwa kwa mbele hivyo tairi kuweza kuacha ardhi na kuelea angani.

sasa tafuta balance point...  huku unavuta mafuta kwa kuyapimia.. bila kusahau breki..(ya nyuma) pale unapoona inazidi kuja juu...
(kasi haizingatiwi sana.. ni best kwa wazee wanaopenda SLOW JAMS..."slow wheeling"
standing wheelie (Don ghb)TZ

unaweza kutumia manjonjo mbalimbali... 
kama KUSIMAMIA... (standing wheelie)
-kupiga mikasi (RINGI)..
Ringi (Salum Tony MONTANA) TZ
pia hata kushusha mguu mmoja chini..na nyingine nyingi.. yote yanawezekana..

JE naweza kutumia pikipiki yoyote kufanya mchezo huu???

JIBU ni ndio/hapana kwa wakati mmoja...
inafaa pikipiki yenye nguvu.. yenye uwezo.. yenye vifaa vilivyo bora na utimamu wa injini...
(slogan ya watu wa dede wanasema HAIKATAI).. wakimaanisha hakuna pikipiki inayowashinda kunyanyua...

Acrobatics (ahmed kalunde)TZ
ANGALIZO..
-hakikisha umevaa nguo nzito kujihami na michubuko ya hapa na pale
-hakikisha unafanya mchezo huu mbali na makazi ya watu.. au mbali na mkusanyiko wa watu (kama unajifunza)
-hakikisha umejikinga kichwa chako kwa kuvaa kofia ngumu..

ni HATARI lakini SALAMA..

sitting wheelie  (Chudy) TZ 
#DAR WHEELIE BOYZ respect
#Kaskazini wheelie boys respect..





unaweza kuuliza swali lolote tutakusaidia

Sunday 16 September 2018

ZIJUE BAADHI YA INJINI za TOYOTA

Toyota V12 Generation
1GZ-FE (5.0L) v12
Kinara=1GZ-FE (5.0L)
ni injini kubwa kuliko zote zilizotengenezwa na TOYOTA ina uwezo wa hali ya juu sana

Toyota V8 Generation
2UZ-FE (4.7L)
Kinara =2UZ-FE (4.7L)
ni injini ya pili kwa ukubwa ambayo imeundwa mahususi kwa matumizi ya OFF -ROADS na utazikuta katika Landcruisers zilizotengenezwa hivi karibuni

Toyota 6 Generetion
2JZ-GTE (3.0L)

kinara=2JZ-GTE (3.0L)
ni injini yenye nguvu sana,na inapatikana miongoni mwa toyota Supra na baadhi ya toyota aristo. pia bila kusahau 1Jz ambayo ina 2.5L inayofanya kazi kwa ufanisi kama v8
zipo zenye VVTI na zilizo hazina VVTI..
pia 2JZ-GE haiko nyuma nayo ni injini inayotamaniwa na wengi
katika miaka ya 80.. toyota waliibuka na 1G-series (2.0L) (1G, 1G-GTE,  1G-GZE)
wakaendelea kushusha vitu.. 1GR-FE VVTI (4.0L) utaipata katika baadhi ya PRADO OFF ROAD.. version ambazo za zamani zilikuja na 5VZ-FE (3.4L)

bila kusahau 3MZ-FE (3.3L) V6 inapatika katika KLUGGER new models pamoja na 1MZ-FE (4.5L) inayopatikana katika CAMRY pamoja na LEXUS300.
 3VZ-FE. ipo katika vichwa vya watu kwa kutoa nguvu ya kutosha..
na mwisho ni 1FZ-FE inayopatikana katika baadhi ya LANDCRUISERS... ni moto

Toyota 4-four Generation
3S-GTE (2.0L)

kinara=3S-GTE (2.0L)
katika ALTEZZA nyingi zina 3S-GE VVTI pia Baadhi ya gari zinatumia 2ZZ-GE(1.8L) ambayo inafahamika kwa ufanisi wake.
4A-series nazo zina ubabe katika 4 Generation... Hapa utakutana na 4A-GE toyota hawakuwa nyuma kuunda injini yenye supercharger ambayo ni 4AG-ZE

Kwa ufupi hizo ni baadhi ya injini zenye ubora wa hali ya juu zilizowahi kutengenezwa na kampuni ya TOYOTA.....

KWA UFUPI...

V12s

1GZ-FE 5.0 litre                                                               206kW



V8s 

3UZ-FE 4.3 litre                                                              206/210kW
1UZ-FE 4.0 litre VVT-i                                                         206kW
1UZ-FE 4.0 litre                                                                 190kW
2UZ-FE 4.7 litre                                                                 170/173kW
5V-EU 4.0 litre                                                                 121kW


6's

2JZ-GTE 3.0 litre twin turbo                                                  206kW
1JZ-GTE 2.5 litre twin turbo/single turbo VVT-i -                185kW
2JZ-GE 3.0 litre                                                                  166kW
1GR-FE 4.0 litre                                                                  179kW
7M-GTE 3.0 litre turbo                                                          173/179kW
3MZ-FE 3.3 litre                                                                  172kW
1FZ-FE 4.5 litre                                                                  165kW
1MZ-FE 3.0 litre VVT-i                                                          158/162kW
1G-GTE 2.0 litre twin turbo                                                  136 - 154kW
1MZ-FE 3.0 litre                                                                  145kW
7M-GE 3.0 litre                                                                  142kW
3VZ-FE 3.0 litre                                                                  139kW
5VZ-FE 3.4 litre                                                                  132kW
1G-GZE 2.0 litre supercharged                                       125kW


4's
3S-GTE 2.0 litre turbo           136 - 191kW
3S-GE 2.0 litre (11.5:1 CR)         154kW
2ZZ-GE 1.8-litre         140/141kW
3T-GTE 1.8 litre turbo         125kW approx
4A-GZE 1.6 litre supercharged         123kW
4A-E 1.6 litre 20-valve         119kW
2AZ-FE 2.4 litre         115kW
1AZ-FE 2.0 litre         110kW
1ZZ-FE 1.8 litre          103kW
4E-FTE 1.3 litre turbo         100kW
4A-GE 1.6 litre         88/100kW
1NZ-FE 1.5 litre                                                              80kW
2T-TELU 1.3 litre turbo         77kW



ANGALIZO; 1 kiloWatt = 1.34102209 hp

Friday 13 July 2018

VIFAA MAALUMU VINAVYOWEZA KUGUNDUA (Tochi) (speedGuns/Speed Radar)

Maendeleo ya sayansi na teknolojia yamekuwa kwa kasi na kuibuka ushindani wa mambo mengi yanayotawala maisha ya binadamu kwa kiasi kikubwa,
mashindano hayo yamepelekea vyombo vya usalama katika nchi mbalimbali kutumia pesa nyingi ili wawe na teknolojia mpya itakayowalahisishia kazi ya kukamata wahalifu mbalimbali,pia wahalifu nao hawako nyuma wao ndio vinara wa kugundua teknolojia mpya ili wasiingie katika mikono ya polisi..

RADAR DETECTORS/vigunduzi vya TOCHI
Kuanzia miaka ya 1970 vifaa hivi vinavyotoa taarifa ya kuwepo ASKARI mwenye Tochi au Tochi iliyotegeshwa kwa dereva aliye kwenye mwendokasi  hivyo dereva huyo kupunguza mwendo wa chombo chake..

kila miaka inavyozidi kwenda Vifaa hivi (TOCHI) vinafanyiwa marekebisho zaidi ili kukamata madereva wasio fata sheria za barabara (mwendokasi)

kwa sasa kuna toleo jipya la hivi vigunduzi vya tochi ambavyo vinaharibu taarifa iliyotakiwa kuchukuliwa na tochi,hivyo tochi kusoma spidi 0 ingawa gari imepita ikiwa na mwendo mkali hata kufikia 180/kph

kwa nchi zilizoendelea zimetoka katika kutumia TOCHI zinazopima kwa kutumia nyenzo ya RADIO WAVES..na kuhamia katika Infraled LIGHT (TOCHI aina ya LIDAR GUN) ambayo hupimwa na LIDAR DETECTOR pekee..
SPEED GUN /speed radar (TOCHI)
Askari wa barabarani anayetumia Tochi(LIDAR GUN) huweza kusoma mwendokasi wa gari husika hata ikiwa umbali wa (mita910) sasa hivi vigunduzi vya LIDAR detector vina uwezo wa kuchanganya (Tochi LDAR GUN) na hatimaye kufeli kusoma spidi husika.. hata kama gari imepita na 180kph kwa polisi itasoma 0kph.


JE SHERIA INARUHUSU VIFAA HIVI?

Jibu ni HAPANA.. na NDIO kwa wakati mmoja, kuna nchi mbalimbali zinaruhusu kumiliki kifaa hiki ila Hauruhusiwi kukitumia katika gari,zipo nchi nyingine hauruhusiwi kumiliki wala kutumia katika gari.

nchi za ukanda wa scandnavia zimeweka sheria kali kutokana na MATUMIZI ya vifaa hivi ikiwemo FAINI kubwa kwa dereva atayegundulika pia kutaifishwa kwa kifaa endapo kitakamatwa na askari wa usalama barabarani...
moja ya kifaa madhubuti kinachotoa taarifa kwa dereva iwapo mbele kuna ASKARI mwenye tochi au TOCHI iliyotegeshwa(radar detector) 


 VIFAA BORA VYA UGUNDUZI WA TOCHI (SpeedRADAR Detectors)
#1 : Uniden R1 & Uniden R3 Radar Detectors
BEI: $299 kwa  R1,
      ; $399 kwa R3 Radar Detector

#2 : Valentine One Radar Detector /w V1Connection or V1Connection LE
BEI: $399 kwa V1,
      ; $49 kwa Bluetooth module,katika iphone/android bure

#3 : Escort Redline EX Radar Detectors
BEI: $599

#4 : Escort Max 360 Radar Detector
BEI: $649, katika iPhone/Android bure ila kwa matumizi kwa ufanisi zaid
 BEI;$49/Ada ya mwaka.

#5 : Radenso XP & Radenso SP Radar Detectors
BEI: $249 kwa SP, 
      ;$399 kwa XP Radar Detector

#6 : Escort iX Radar Detector
BEI: $399

#7 : Radenso Pro M Radar Detector
BEI: $549

#8 : Uniden DFR7 & Uniden DFR6 Radar Detectors
BEI: $399 kwa DFR7,
      ; $299 kwa DFR6

#9 : Escort X80 Radar Detector
BEI: $299

#10 : Whistler CR93 & Whistler CR88 Radar Detectors
BEI: $279 kwa CR93, 
      ;$229 kwa CR88

Honorable Mention: Cobra DSP-9200BT Radar Detector
BEI: $299





Thursday 12 July 2018

Historia ya VW Beetles (people's car)


Hizi ni gari zinazovutia sana macho ya watu wengi,kwa Tanzania zimepotea kwa kiasi kikubwa kutokana na kufurika kwa magari ya kisasa kutoka katika nchi mbalimbali ikiwemo JAPAN kuwa ndio kinara wa kuleta gari nyingi sana..

Chimbuko la VW

huwezi kuamini,ila ukweli ndio huu,katika miaka ya 1924 Mwamba wa DUNIA Adolf Hitler alipata wazo la kutengenezwa kwa gari hizi akiwa GEREZANI..
Hitler aliwaza mengi ikiwemo kupunguza Tatizo la ajira katika nchi yake,pia Gari hizi zingeweza kununuliwa na watu wengi hasa wale wenye Uchumi wa kati na wachini pia,ndio maana VolksWagen huitwa (peoplea's car) yaani 'Gari ya watu'.
ilipofikia miaka ya 1933 Chama cha NAZI kiliingia madarakani na Hitler jambo lake la kwanza ni kuwepo kwa barabara maalum kwa ajili ya magari,na alifanikiwa kufanya hayo na ndoto yake ilikamilika MWAKA 1939.

Zoezi zima la KUUNDWA kwa VW

Ferdinand Porsche,ambaye ndiye mmiliki wa kampuni ya Kubuni na kudizaini magari,iliyopo STUTTGART Germany alipewa kibarua kizito na Adolf hitler akamilishe ndoto yake ya kutengeneza gari muhimu ndani ya miezi kumi.. kibarua hicho alipewa 1934... na hakumuangusha Bosi wake alidizain vile Hitler alivyotaka...

yafuatayo ni maagizo aliyompa bwana ferdinand Porsche...

-gari inatakiwa iwe na uwezo wa kukimbia; 62Mph.
-gari iwe na uwezo wa kwenda miles (maili) 45 kwa lita 5.
-gari inatakiwa iwe na injini yenye mfumo wa kupoza kwa kutumia Hewa.
-pia iwe na uwezo wa kusafirisha watu wazima wawili na watoto watatu.
-na jambo la mwisho alilosisitiza ni kuwa gari lazima iuzwe bei isiyozidi £8.

UCHAMBUZI WA VW beetle (Overview)
>Adolf hitler alisisitiza matumizi ya injini inayopoozwa kwa upepo kuliko injini inayopoozwa kwa Maji kwasababu injini inayopoozwa kwa upepo ni Nyepesi kulinganisha na hii injini nyingine..
>Volkswagen Beetle (1938-1979) Kipindi hicho chote, ilishika nafasi ya pili kwa kuwa ndiyo Gari iliyouzwa kwa wingi Duniani kwa ujumla
>jumla ya Magari milion 21 yalitengenezwa Duniani kwa ujumla
>Hizi gari zina tambulika kuwa injini yake inakaa nyuma,hivyo kumpa dereva uwezo wa kukata kona kiurahisi bila ya kutumia nguvu nyingi,pia mbele kuna nafasi inayotumika kuweka mizigo pia katika siti kwa nyuma kuna nafasi kubwa tu ya kuweka mizigo mbalimbali.
>1959 katika bara la AMERIKA ilishika nafasi ya kwanza kwa magari ya kigeni yaliyouzwa barani humo..
MATOLEO mbalimbali ya BEETLES
(inapaswa kuzingatiwa kuwa kabla ya vita ya pili ya Dunia Kila nchi Barani ulaya ilijipanga kikamilifu.. hali iliyochangia Hitler kuimalisha safu yake ya jeshi kwa kuundwa kwa beetle maalum kwa matumizi ya jeshi tuu... na ni kwa wanajeshi walio na beji ya VIP.. gari hii ni Kommandeurwagen or type 87  Toleo lijalo nitaichambua gari hii kiundani zaidi maana ina maajabu ya kipekee)
1-Type 82 Kubelwagen ---boat mode
2-Type 166 Schwimmwagen
3-Kommandeurwagen or type 87  
zipo zingine nyingi
-Volkswagen AutoStick 1967 ulaya/1968 Marekani (kama tunavyowajua wamarekani wanavyopenda URAHISI, miaka yote nyuma beetles zilikuwa ni (manual) ila kipindi hiki waliona watoe beetle yenye uwezo wa kutumika kama manual na automatic gari hizi zilikuwa hazina (clutch pedal)..
-Super Beetle ilitengenezwa 1971 mpaka 1979
-Beetle Convertible hii iliundwa katika miaka ya 1953

ingawa gari hizi zinatambulika kuwa na nguvu ndogo,zilipendwa na wengi kwa sababu ni rahisi kuzimudu katika masuala ya mafuta,vipuri (spea) ni rahisi kununuliwa na mambo mengine mengi.


Kupotea Kwa Beetles katika Ramani ya DUNIA
-HADI kufikia miaka ya 1970's ushindani wa kutengeneza magari ya kiuchumi (yasiyotumia mafuta mengi) ulizidi kwa kasi kutokana na wamerekani na wajapani kuingilia soko hili la magari kwa nguvu kubwa sana

wamerekani walikuja na aina mpya ya gari ambayo ni Chevrolet Vega na Ford Pinto ambazo zilipendwa na atu wengi kutokana na kutumia mafuta kwa kiasi kidogo,mauzo ya beetles yalishuka kwa asilimia 50%

viwanda mbalimbali viliacha na vingine kupunguza uzalishaji wa beetles nchini ujerumani hadi kufikia miaka ya 1979 ingawa walichechemea kutengeneza gari hizi hadi 1980 ili kukamilisha oda mbalimbali walizopokea duniani kote.

Mwisho..
>>>> Wafanyabiashara na wateja wengi wa beetles waliibukia nchini MEXICO na kuendelea kutengeneza gari hizi miaka ya 1981 kufikia idadi ya gari milioni 20 kutengenezwa katika Ardhi ya mexico..
hadi kufikia hivi leo MEXICO ndio nchi Pekee inayotengeneza gari aina Beetles
na gari hii iliteka hisia za wengi na kupelekea kupigiwa kura na wananchi wa MEXICO kuwa ndio gari pendwa ya nchi yao kuliko gari nyingine yoyote ile katika karne Hii.